MSANII nyota wa filamu nchini, Single Mtambalike 'Richie' anatarajia kuingiza sokoni, filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Diana.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Richie, alisema ameshamaliza kurekodi filamu hiyo ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni.
Alisema filamu hiyo inatarajia kuwa ya aina yake kutokana na maudhui aliyotumia kupeleka ujumbe kwa jamii.
Richie alisema katika filamu hiyo, amewashirikisha wasanii mbalimbali wakiwemo wakongwe na chipukizi, ili kuleta ladha tofauti.
Alisema filamu hiyo inatarajia kufanya vizuri sokoni, kwani imebeba ujumbe mzito na matatizo mbalimbali ambayo yanatokea katika jamii kila siku.
“Nimeshakamilisha filamu yangu mpya, ambayo inatarajia kuingia sokoni hivi karibuni na filamu hiyo najua mashabiki wangu wataipenda, kutokana na maudhui iliyonayo,” alisema.
Na Victor Mkumbo
- MSANII nyota wa tasnia ya filamu nchini, Kurwa Kikumba 'Dude' anatarajia kuingiza sokoni filamu ya Bongo Movie mwezi Februari mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam, Dude alisema kuwa anatarajia kuingiza sokoni filamu hiyo baada ya kupokea maombi mengi kutoka kwa mashabiki wake.
Alisema kuwa Bongo Movie ni moja ya tamthilia iliyoweza kumpandisha chati msanii huyo kutokana na matukio ya utapeli aliyokuwa akiyafanya.
Dude alisema kuwa ameshaanza kurekodi baadhi ya vipande kwa ajili ya kukamilisha filamu hiyo inayopedwa na watu wengi.
Alisema kuwa filamu moja ya Bongo Movie, itachukua muda wa saa 1:30, kutokana na uzito wa tukio husika.
“Ninatarajia kuingiza sokoni filamu yangu ya Bongo Movie baada ya kupata maombi mengi kutoka kwa wadau wa filamu nchini” alisema.
Msanii huyo ambaye anaigiza kama tapeli, alisema kuwa tamthilia za kuuza kwenye vituo vya televisheni hazilipi hivyo ni bora aingize videoni ili aweze kuuza kwa kiasi kikubwa.
Na Victor Mkumbo
No comments:
Post a Comment