Monday, February 13, 2012

ROSE MUHANDO KATIKA MKATABA MNONO NA SONY MUSIC


Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla,Rose Muhando(pichani), hapo jana imewekwa wazi kwamba ameingia mkataba mnono na kampuni mahiri katika masuala ya muziki na burudani hapa ulimwenguni,Sony Music.
Rose Muhando ambaye anakuwa msanii wa kwanza wa muziki wa injili nchini Tanzania kuingia mkataba wa namna hiyo na Sony Music,atasimamiwa kutoa album tano hiyo ikiwa ni katika suala zima la uandaaji na usambazaji.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Biashara wa Sony Music,Russell Crawford,kampuni yake imedhamiria katika kuwawezesha wasanii wa hapa nyumbani kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa wasanii mbalimbali duniani ikiwemo wale maarufu kama vile Usher, Chris Brown, Toya Delazy, Beyonce, Pitbull, Tumi and the Volume, J Cole and R Kelly.
BC inapenda kutoka pongezi nyingi kwa Rose Muhando na timu yake yote.

Photo Credit:Global Publisherz

Read more: BongoCelebrity

1 comment:

  1. HIYO GAUNI ALIYOVAA ROSE MHANDO NI YA PART AU NI YA KUIMBA KWAYA? UTAFIKIRI ANAIMBA BONGO FLEVA?

    ReplyDelete

Labels