Monday, February 13, 2012

WHITNEY HOUSTON AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 48

 Breaking News

Mwimbaji na muigizaji maarufu kutoka nchini Marekani,Whitney Houston,amefariki dunia muda mfupi uliopita(Jumamosi mchana saa tisa na dakika hamsini na tano kwa saa za Marekani-Pacific) akiwa na umri wa miaka 48. Whitney Houston ambaye ni miongoni mwa waimbaji waliokuwa na kipaji cha aina yake katika uimbaji,amekutwa na walinzi wake wa karibu(bodyguards) akiwa hajitambui katika gorofa ya nne ya chumba cha hotel ya The Beverly Hilton alipokuwa amefikia. Watu wa dharura walijaribu kuokoa maisha yake bila mafanikio na hivyo ikatangazwa rasmi kwamba amefariki.

Whitney ambaye alikuwa na kipaji cha aina yake katika uimbaji,amefariki dunia katika mkesha wa tuzo maarufu za Grammy na alikuwa amepangwa kutoa burudani katika party ya Clive Davis,producer na music mogul ambaye amekuwa na Whitney Houston tangu alipoanza  muziki.
Kwa muda mrefu,Whitney Houston, ambaye aliwahi kuolewa na mwanamuziki mwingine maarufu,Bobby Brown(walizaa mtoto mmoja Bobbi-Kristina Brown baada ya kuoana mwaka 1992 na kuachana mwaka 2007) amekuwa na tatizo la utumiaji wa madawa ya kulevya.Aliwahi kutunukiwa Udaktari wa Heshima kutoka Granning State University cha huko Lousiana.

PUMZIKA KWA AMANI WHITNEY!

No comments:

Post a Comment

Labels