Thursday, February 2, 2012

Richie kuingiza Diana sokoni

MSANII nyota wa filamu nchini, Single Mtambalike 'Richie' anatarajia kuingiza sokoni, filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Diana.



Akizungumza Dar es Salaam jana, Richie, alisema ameshamaliza kurekodi filamu hiyo ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni.

Alisema filamu hiyo inatarajia kuwa ya aina yake kutokana na maudhui aliyotumia kupeleka ujumbe kwa jamii.

Richie alisema katika filamu hiyo, amewashirikisha wasanii mbalimbali wakiwemo wakongwe na chipukizi, ili kuleta ladha tofauti.

Alisema filamu hiyo inatarajia kufanya vizuri sokoni, kwani imebeba ujumbe mzito na matatizo mbalimbali ambayo yanatokea katika jamii kila siku.

“Nimeshakamilisha filamu yangu mpya, ambayo inatarajia kuingia sokoni hivi karibuni na filamu hiyo najua mashabiki wangu wataipenda, kutokana na maudhui iliyonayo,” alisema.

Na Victor Mkumbo

No comments:

Post a Comment


Labels