Sunday, February 5, 2012

Mitindo ya nywele


Mitindo ya nywele inapompendezesha mwanamke
Na Rehema Maigala

KARIBUNI wapenzi wasomaji wetu wa safu hii muipendayo ya urembo, leo katika safu hii nimewaandalia mitindo mbalimbali ya nywele ambayo inayomfanya mwanamke kuonekana amependeza.

Kila mwanamke ana nywele na nywele zinamfanya mwanamke kubadili sura yake na kuonekana  amependeza kwani kila mtindo wa nywele unamfanya mwanamke kupendeza.


Kwa kuwa nywele ni kiungo kikubwa kwa mwanamke ndio maana wanawake wengi wanapenda kupendezesha nywele zao ili waonekana kupenda zaidi ya mwingine.

Wanawake wengi wanatumia pesa nyingi kwa ajili ya kupendezesha nywele zao.
Kuna mitindo mingi ya nywele inategemea muhusika anapendelea nywele zake kuonekana vipi ili azidi kupendeza.Mwanamke anaweza kuvaa vazi zuri lakini kama nywele zake zikiwa hazijapendeza haonekani kama amependeza.

Mitindo ya nywele ipo mingi kama, kunyoa, kusuka rasta, kubana kwa aina tofauti, kuzichana na kusuka hiyo yote ni mitindo ya nywele hapo mwanamke huchagua hupendelea nywele zake kuziweka vipi ili aonekane kapendeza zaidi ya mwenzake.

Mara nyingi tunasema kuwa mitindo ya nywele humbadilisha mtu , nikweli unaweka kusuka nywele na ukaonekana umependeza zaidi ya huyo aliyebana.

Pia nywele zinamatunzo yake ndio maana huonekana kupendeza zaidi, matuzo yake ni kama, kuosha nywele na sabauni inayostaili .

Mwanamke ukiwa na utaratibu wa kuosha nywele zako haziwezi kuwa na mba au wadudu wengine wanaopenda kuishi katika nywele chafu.

Wapo wakina mama ambao huwa na mvi katika nywele zao lakini kwa kuwa wanazipenda hupaka dawa ya rangi nyeusi nayo pia dawa hiyo hufanya nywele za mwanamke kupendeza na kubadilisha sura ya mwanamke huyo.

Hakuna duka la urembo lililopo sehemu yeyote linalouza bidhaa za urembo bila ya kuuza nywele za bandia za wanawake ni kwa sababu zinasoko kubwa .

Watoto wadogo  nao wanapendeza kufuga nywele ili mradi tu mzazi au mlezi uwe msafi kuzipendezesha nywele hizo ili zionekana kuwa ni nzuri na safi zaidi.

Watoto wa kike wanapendeza zaidi kama nywele zao zikibanwa na vibanio vya kitoto.
mwisho...
 

No comments:

Post a Comment

Labels