Saturday, December 17, 2011
WANANCHI WAELIMISHWE KUHUSU MFUMO WA DIGITALI
Naibu
Waziri wa Sayansi na Teknolojia ,Bw Charles Kitwanga ameyashawishi
mataifa ambayo tayari yamejiunga na mfumo wa Digitali katika harakati za
kuharakisha mawasiliano bora duniani kutumia nafasi hiyo kutoa ubunifu
wao na ikiwezekana kuyasaidia yale ambayo ndiyo yanaanda ili waweze
kufikia lengo la pamoja kwa wakati.
Changamoyo
hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Arusha wakati akifungua
mkutano wa sita wa Mamlaka za Mawasiliano wa nchi za Afrika (ACRAN)
unaoshirikisha nchi zaidi ya 20 wanachama wa jumuia hiyo kwa niaba ya
Waziri wa wizara hiyo Bw Makame Mbarawa.
Kitwanga
aliwataka wataalamu hao ambao nchi zao tayari zimeingia kwenye mfumo wa
digitali kusaidia mataifa ambayo yanaelekea kujiingiza katika mfumo
huo.
Tanzania
hasi kufikia Disemba mwakani mashirika yote yanatakiwa yawe yanatumia
mfumo wa digitali na kuachana na analogia hivyo ni wajibu wa wadau
mbalimbali kuwaelimisha wananchi namna ya kutumia mfumo huo.
Mashirika ambayo yamepewa dhamani ya kuuza ving'amuzi ni pamoja na Star Times,Ting Agape TV, Sahara Communication na IPP Media
kuimba unaweza kujifunza!bt sauti ni muhimu.
ReplyDeletekuimba unaweza kujifunza!bt sauti ni muhimu.
ReplyDelete