Watayarishaji wa
party hiy wakionesha DVD ya kitchen party gala iliyopita ambazo
wanatarajia kuzitengeneza kwa wingi na zitaanza kupatikana mapema mwezi
ujao,ambapo kila mwezi watakuwa wakirekodi,kwa wale watakaotaka kununua
labda alipitwa zitakuwa zikipatikana.
Women In Balance-kitchen party Gala
Wasichana
na wanawake wengi kwa sasa wanakabiliwa na changamoto nyingi sana
ambazo zinapelekea kushindwa kusimama katika mahusiano
yao.Teknolojia,mwamko wa elimu,wanawake kumiliki biashara
binafsi,kazi,wazazi hawahusishwi ,kila mtu mjuaji ,kujisahau n.k
Matokeo
yake talaka nyingi na mahusiano kuvunjika sasa tunataka kumkumbusha
mwanamke wajibu wake na nafasi yake katika mahusiano.Ajitambue.
Msimu wa pili
Eneo
hili limelenga kukuza ujuzi wa mwanamke katika Nyanja za kijamii
zaidi.Kupitia eneo hili mwanamke atajifunza mambo mbalimbali kiasili na
kisasa ambayo mwanamke anaengia au aliyeko au anaetegemea kuingia
katika mahusiano na ndoa.Mambo kama malezi ya watoto ,nafasi yake
katika jamii umuhimu kujiamini na mengineyo.
Wazo
hili limekuja mara baada ya kuona kwamba ule muda wanawake wanaopata
kuongea mambo haya kwenye kitchen party ni mchache na
hautoshi kumfahamisha mwanamke mambo yote muhimu.Mambo ambayo ni
lazima ayajue au hata kama anayajua kutokana na pilika pilika za maisha
anajisahau.
Tukio
hili kufanyika jumamosi hii ya tarehe 28 january 2012.Kuanzia saa nane
mchana mpaka saa mbili usiku katika ukumbi wa Danken house uliopo
mikocheni kwa warioba.
Watoa mada ni watu wenye uwezo katika swala zima la uelimishaji
Aunt sadaka;Ni
mwana saikolojia aliyebobea katika maswala ya wanawake na watoto.Ana
uwezo katika Nyanja hii ambao umetokana kielimi na uzoefu wa kukutana na
kesi mbalimbali amabazo zinazo mguza mwanamke hivyo kuweza kuwa funzo
kwa wengine.
Bi Chau ni
mwanamke ambae mbali na kuwa katika fani ya sanaa kwa muda mrefu
wamekua wakito amafunzokwa wanawake tokea muda mrefu.Mafunzo ya
mahusiano,ndoa na familia kwa ujumla.
Mama Victor;Ni
mtumishi wa Mungu katika dini ya kikristo ambae anaelimisha wanawake
kwa mafunzo ya kidini.Anafundisha mwanamke kujitambua vile mungu amempa
uwezo wa kuitumikia jamii yake kama mlezi na kiongozi.
Kwa ufupi hawa ndio wakufunzi katika tukio letu hili la women in Balance jumamosi hii katika msimu wa pili.
Burudani itatolewa na Nyota Waziri.
Huu
ni mkakati wa mwaka mzima huu 2012 na tutakutana kila mwezi mpaka mwezi
march ambapo ratiba itabadilika na wanaume kuhusishwa.
WADHAMINI WETU WA SIKU HII NI
BAILEYS (kinywaji),MGen insuarance,cocacola,cooperate image na clouds fm.
IMETOLEWA NA MRATIBU WA WOMEN IN BALANCE
DINA MARIOS.
Big up 4all!hiyo ni gud ideas.
ReplyDelete