Thursday, February 2, 2012

Profesa Mwandosya arudi India

*Dkt. Mwakyembe aonekana ofisini mara moja

WAZIRI wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, ameondoka nchini juzi kwenda India
ili kuangalia maendeleo ya afya yake ambapo Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, akidaiwa kuripoti ofisini mara moja tangu arejee nchini.

Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha habari Wizara ya Maji, Bw. Nurdini Ndimbe, alisema tangu arejee nchini, Prof. Mwandosya anaendelea vizuri.
Lengo la safari ya India ni kwenda kuangalia maendeleo ya afya yake kwani alitakiwa kurudi nchini humo baada ya mwezi mmoja kuonana na daktari wake, hatujui atarudi lini,¡± alisema.
Kwa upande wake, Bw. Makyembe kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya Wizara hiyo, vinasema tangu alipotoka nchini India, aliingia ofisini mara moja na kufanya kazi zake.
Kuhusu maendeleo ya afya yake naomba mumuulize msemaji wa familia ambaye ni Mbunge wa Lupa, mkoani Mbeya Bw. Victor Mwambalasa, yeye ndiye anaweza kuzuingumzia hili,¡± kilisema chanzo chetu.
Hata hivyo, juhudi za gazeti ili kumpata Bw. Mwambalasa ziligonga mwamba ambapo Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Bladina Nyoni, alipoulizwa kuhusiana ugonjwa unaomsumbua, Dkt. Mwakyembe alisema, hiyo ni siri yake na daktari wake.Hakuna mtu anayeweza kusema ugonjwa wake labda yeye mwenyewe, alisema Bi. Nyoni.
Hivi karibuni Dkt. Mwakyembe alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa, ripoti ya ugonjwa unaomsumbua tayari imetumwa serikalini.

Na Gladness Mboma

No comments:

Post a Comment


Labels