Thursday, February 2, 2012

Bongo Dar es Salaam kurudi tena

MSANII nyota wa tasnia ya filamu nchini, Kurwa Kikumba 'Dude' anatarajia kuingiza sokoni filamu ya Bongo Movie mwezi Februari mwaka huu.Akizungumza Dar es Salaam, Dude alisema kuwa anatarajia kuingiza sokoni filamu hiyo baada ya kupokea maombi mengi kutoka kwa mashabiki wake.

Alisema kuwa Bongo Movie ni moja ya tamthilia iliyoweza kumpandisha chati msanii huyo kutokana na matukio ya utapeli aliyokuwa akiyafanya.

Dude alisema kuwa ameshaanza kurekodi baadhi ya vipande kwa ajili ya kukamilisha filamu hiyo inayopedwa na watu wengi.

Alisema kuwa filamu moja ya Bongo Movie, itachukua muda wa saa 1:30, kutokana na uzito wa tukio husika.

“Ninatarajia kuingiza sokoni filamu yangu ya Bongo Movie baada ya kupata maombi mengi kutoka kwa wadau wa filamu nchini” alisema.

Msanii huyo ambaye anaigiza kama tapeli, alisema kuwa tamthilia za kuuza kwenye vituo vya televisheni hazilipi hivyo ni bora aingize videoni ili aweze kuuza kwa kiasi kikubwa.

Na Victor Mkumbo

1 comment:

  1. NAISUBIRI KWA HAMU HIYO, DUDE NAMKUBALI MEEEEEEEEN

    ReplyDelete

Labels