
Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Tanzania na Afrika kwa
ujumla,Rose Muhando(pichani), hapo jana imewekwa wazi kwamba ameingia
mkataba mnono na kampuni mahiri katika masuala ya muziki na burudani
hapa ulimwenguni,Sony Music.
Rose Muhando ambaye anakuwa msanii wa kwanza wa muziki wa injili
nchini Tanzania kuingia mkataba wa namna hiyo na Sony Music,atasimamiwa
kutoa album tano hiyo ikiwa ni katika suala zima la uandaaji na
usambazaji.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Biashara wa Sony Music,Russell
Crawford,kampuni yake imedhamiria katika kuwawezesha wasanii wa hapa
nyumbani kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa wasanii mbalimbali duniani
ikiwemo wale maarufu kama vile Usher, Chris Brown, Toya Delazy, Beyonce,
Pitbull, Tumi and the Volume, J Cole and R Kelly.
BC inapenda kutoka pongezi nyingi kwa Rose Muhando na timu yake yote.
Photo Credit:Global Publisherz